Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali Petro Ngata wakionesha mkataba wa ushirikiano wa utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia mara baada kuusaini. Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma, mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 50.98 imesainiwa kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na taasisi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Magereza (TPS) na Wasambazaji wa Gesi ya kupikia, hafla ambayo ilienda sambamba na uzinduzi wa jengo la REA.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga akigawa mtungi wa gesi kwa mmoja wa wananchi katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga wakati wa hafla ya kugawa mitungi ya gesi na majiko banifu iliyofanyika tarehe 17 Mei, 2024
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizindua kituo cha umeme cha Ifakara wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
11 EAST AFRICAN PETROLEUM CONFERENCE AND EXHIBITION (EAPCE'25)
Baadhi ya mitambo ya umeme katika kituo cha kupoza umeme cha Mpomvu kilichopo mkoani Geita.